Kwanini nijiunge Ajiras wakati biashara yangu inawateja tayari?

Ajiras ni mtandao unaokuwezesha kujiajiri kwa kuuza huduma mtandaoni kwa mamilioni ya watu popote walipo. Kama mitandao mingine, kuendesha mtandao mkubwa kama huu una gharama zake. Lakini vilevile tukumbuke pia Ajiras ni biashara na kuwa inalipa kodi mbalimbali kulingana na sheria za kodi za Tanzania.
Kwanini utumie Ajiras
-
Uwezo wa wateja kuandika sifa (reviews)
Swali hili lina majibu mengi. Pengine naweza kujibu hili swali kwa kukuuliza swali.
- Je umeshafanya kazi ngapi nje ya mtandao wa Ajiras?
Bila shaka, wengi wenu mmefanya kazi nyingi sana. Na pia unawateja wako ambao wanakupa kazi mara kwa mara.
- Nini sheria ya kwanza ya kuwezesha biashara idumu?
Tunaweza pishana kwenye hili ila ukweli ni kwamba, sheria ya kwanza ni uwezo wa biashara yako kukua na kuongeza wateja.
- Unawezaje kuongeza wateja?
Wengi hasa biashara ndogo ambazo hazina uwezo wa kutangaza kwenye luninga na redio, tunategemea wateja wako kuwaleta ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa hiyo ukuaji wa biashara yako hutegemea wateja wako kukuletea wateja wengi. Na hii ni kuwa wanatoa sifa (review) nzuri ya huduma uliyompa mteja. Tumeutumia mfumo huu mwa muda mrefu na umetufaa kaisi flani. Lakini kama tunavyojua, nyakati zinabadilika, njia hii sasa hautuletei wateja wengi kama zamani au kama tunavyotarajia. Tatizo moja wapo ni kuwa sifa (review) hizo anazitoa kwa mdomo na kwa watu anao faamiana nao tu. Ina maana upatikanaji wa wateja wanaoletwa na wateja wengi hutegemea sana na idadi ya watu anao faamiana nao. Kwanini tusiongeze hiyo idadi na kuwafikia hata watu wasiofahamiana na wateja wako?
Ajiras ina mfumo unaoruhusu kila mteja wako kutoa sifa (review) kwa kazi uliyomfanyia. Sifa hizo, zitaonekana na kusomwa na watu wote wataoingia ajiras kwenye kazi yako. Embu fikiria hili, kama kazi ulizofanya mpaka sasa, wateja wako wange andika ni kiasi gani wamefurahishwa na kupendezwa na huduma yako, yangeweza kukuletea wateja wengine wangapi? Wateja wapya ambao hawana undugu wala urafiki na wateja wako wa sasa?
Kumbuka, ajiras inatembelewa na maelfu ya watu. Katika maelfu hao huwezi pata angalau 100 kwa kuanzia? Wateja wanapenda kuondolewa wasiwasi, kwaona watu wengine washatumia na kuridhika na huduma zako. Ndio maana hata kama kuna maduka mawili yanauza bidhaa au huduma moja na bei za kufanana. Lakini duka moja lina watu wachache wasubiri huduma wakati lingine lime jaa mpaka foleni, watu bado watenda kwenye lile lenye watu wengi.
Watu wanahitaji kuona wenzeo wamenunua huduma yako na wamefurahishwa nayo. Idadi ya sifa zinapoongezeka vivyo vivyo idadi ya wateja inapoongezeka. Hii ni kwakua inawapa wateja imani kwenye huduma yako.
Kwa hiyo basi, kwa kuuza huduma yako kwenye mtandao wa ajiras, wateja wako wataweza andika sifa (review) na wewe utaweza kuzijibu hizo sifa kwa kuwashukuru wateja wako. Hii inasaidia pia kuonyewa hali ya kuwajali wateja wako.
Kama unatarajia biashara yako kukuwa, mtandaoni ndo sehemu pana yakukuwezesha kukuwa.
Kwa leo tunaishia hapa. Usikose makala nyingine ambayo itaendelea kukupa sababu nyingine ya kwanini utumie mtandao wa ajiras. Sababu zikiwemo kwanini Ajiras na siyo Instagram ama Facebook?
Karibu Ajiras – Soko huru la huduma.